Zaidi ya wazazi 300 wilayani Nkasi mkoani Rukwa wamefikiwa na elimu ya uhamasishaji wanafunzi Kwenda shule kupitia kampeni maalamu ilioandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo ndugu Afraha Hassan.

Aidha, kampeni hiyo imelenga kuwajengea uwezo wazazi na walezi kuweza kutambua umhimu wa kuwapeleka Watoto shule kuanzia elimu ya msingi na sekondari huku shule 30 katika kata 15 zikifikiwa na elimu hiyo.

Awali akiongea na wazazi na walezi kwenye vijiji hivyo,Afisa dawati la msaada wa kisheria ndugu Damas Mwanakatwe, alisema lengo la kampeni hiyo ni kuwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka Watoto shule ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kuwaozesha Watoto katika umri mdogo.

‘’kumekuwa na uelewa mdogo kwa wazazi hasa wafugaji na wakulima kuwa na Imani potofu za kutowapeleka Watoto shule hasa kwa kipindi hiki ambapo shule zimefunguliwa’’ alisema Mwanakatwe.

 Kwa upende wake Afisa usatawi wa jamii wilayani humo ndugu Jackson Bolingo alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kutambua haki za watoto ikiwemo kuzingatia sheria ya mwaka 2009 ambayo inawataka wazazi na walezi kutoa huduma bora kwa Watoto ikiwemo kuwapatia elimu na mahitaji muhimu