Balozi wa China Chen Mingjian, ametembelea Mkoa wa Rukwa katika ziara inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania, hususan katika sekta ya madini na maendeleo ya kijamii.
Katika ziara hiyo, balozi huyo alipata fursa ya kutembelea shughuli mbalimbali zinazoratibiwa na Tume ya Madini katika Mkoa wa Rukwa, ambapo alijionea juhudi zinazofanyika katika kusimamia rasilimali za madini pamoja na fursa zilizopo kwa wawekezaji.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Balozi Chen Mingjian ameeleza kuwa China inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Tanzania, na ipo tayari kushirikiana zaidi katika uwekezaji wa sekta ya madini, utafiti pamoja na teknolojia za uchimbaji.
Akuzungumza na waandishi wa habari Afisa Madini Mkoa Egn:Joseph Kungura Ameeleza kuwa ziara hiyo ni muhimu katika kufungua milango ya uwekezaji na kubadilishana uzoefu, hali itakayochochea ukuaji wa sekta ya madini nchini.
Amesema Kuwa serikali ya china imeridhika na uchenjuajiwa madini ya kopana na kuhaidi kuweka mtambo mkubwa wa uchenjuaji na uchakati wa madini hayo.
Aidha mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa charles Makongoro Nyerere amesema kuwa ujio huo utaongeza uwekezaji mkubwa kati ya tanzania na china ,huku akiongezakuwa sheria ya madini iliyopo inafaa ila ifanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ili kuongeza pato la Taifa.
Kwakipindi cha mwaka 2024/25 idadi ya leseni zilizotolewa ni 175 kati ya hizo leseni za uchimbaji mdogo (MPL) ni 168,leseni za utafiti (PL)1 leseni ya mnunuzi mdogo wa madini (BL) 6 .

Tunapatikana Kupitia