Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama Mei 9, 2026 amewaagiza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wilayani Karagwe Mkoani Kagera kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje kwa lengo la kujenga taswira nzuri kwa wananchi.

CP Mkama amewaagiza watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto, wazazi na walezi kuwalinda na kuwakuza watoto wao katika Maadili yaliyo mema jambo ambalo litapelekea ukuaji wa Jamii mazuri. 

Sanjali na hilo, CP Mkama, amewataka wazazi na walezi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia njia sahihi ili ziwezwe kutekelezwa na kutatuliwa kwa wakati badala ya kupeleka taarifa sehemu ambayo sio rasmi.

Vilevile,  amewaagiza Askari Polisi wa wilaya ya Karagwe na Kagera kwa ujumla kutoa na kuendeleza ushirikiano kwa wananchi lengo likiwa ni kudumisha uhusiano baina Jeshi la Polisi na wananchi. Kufanya hivyo, itapelekea mwananchi kufikisha taarifa pasipo kuwa na uoga wowote